The House of Favourite Newspapers
gunners X

Ole agoma kumpiga benchi De Gea

Ole Gunnar Solskjaer

KOCHA Ole Gunnar Solskjaer ameeleza kuwa hayupo tayari kumuweka benchi kipa wake, David de Gea licha ya kuwa amekuwa akifanya makosa kadhaa na kuruhusu mabao ambayo yanaonekana ni mepesi.

 

Kocha huyo amesema hayo ikiwa ni muda mfupi kabla ya mchezo wa timu hiyo dhidi ya Chelsea, kesho Jumapili katika Ligi Kuu ya England ‘Premier League’.

 

De Gea amekuwa akishutumiwa kucheza chini ya kiwango katika mechi dhidi ya Arsenal, Barcelona, Everton na Manchester City.

David de Gea

Kipa huyo hajamaliza mechi bila kuruhusu bao (clean sheet) kwa miezi miwili sasa na ndiye kipa wa kwanza wa United kufungwa mabao 50 katika Premier League kwa miaka 40 iliyopita. Alipoulizwa kama De Gea atawekwa benchi katika mchezo wa kesho utakaopigwa kwenye Uwanja wa Old Trafford, Solskjaer alisema: “Hapana, hapana kabisa.

 

Namuamini David, kwangu mimi huyu ni mchezaji bora ambaye United imekuwa naye kwa miaka sita au saba iliyopita. ‘’Amekuwa bora na amepitia changamoto nyingi. David atarejea katika ubora wake.” Kumekuwa na taarifa kuwa kukwama kwa mazungumzo ya mkataba wake imekuwa sababu ya kushuka kiwango kwa De Gea, hivi karibuni.

Comments are closed.