The House of Favourite Newspapers

Ole Apotezea Siti ya Mourinho, Achukua ya Ferguson

Ole Gunnar Solskjaer

KOCHA Ole Gunnar Solskjaer ameamua kutumia staili ya ukaaji kwenye benchi la wachezaji kama ilivyokuwa ikifanywa na nguli wa timu yake ya Manchester United, Sir Alex Ferguson.

 

Wakati wa utawala wa kocha Jose Mourinho ndani ya klabu hiyo alikuwa akipendelea kukaa siti za mbele ndani ya Uwanja wa Old Trafford, lakini Ole amekuwa tofauti kwa kufanya kama alivyokuwa akifanya Ferguson kwa kukaa siti ya nyuma na juu.

Hilo lilithibitika wiki iliyopita ambapo Ole alimtoa staa wa timu yake, Alexis Sanchez katika siti ya juu baada ya mchezaji huyo kutolewa. Siri mojawapo ya kufanya hivyo ni kutazama mchezo vizuri na kuwafanya wachezaji wa kwenye benchi kuwa makini na mchezo kwa kuwa wanajua bosi wao yupo nyuma anawatazama.

Comments are closed.