The House of Favourite Newspapers

Ommy Dimpoz achomoa kolabo na Patoranking

0

ommyMkali wa muziki wa Bongo Fleva, Omari Nyembo ‘Ommy Dimpoz’.

Mayasa Mariwata
LICHA ya tetesi kuenea kuwa mkali wa muziki wa Bongo Fleva, Omari Nyembo ‘Ommy Dimpoz’ yupo mbioni kufanya kolabo na staa kutoka Nigeria, Patrick Nnaemeka Okorie ‘Patoranking’ mkali huyo ameibuka na kukanusha vikali.

Akichonga na Amani, Dimpoz anayetesa na Kibao cha Wanjera alisema kuwa tetesi hizo hazina ukweli na wala hana mpango huo kwa sasa.

Patoranking“Hakuna ukweli wowote, sijawahi kuwasiliana na Patoranking wala kutaka kufanya naye kolabo japokuwa kama itakuja kutokea nikalazimika kufanya hivyo nitafanya,” alisema Dimpoz.

Patoranking anatarajiwa kutua ndani ya Dar, Novemba 25, mwaka huu ambapo atafanya shoo katika Fukwe za Escape One,
Mikocheni Novemba 27.

JIUNGE NA GLOBAL BRAKING NEWS

GLOBALBREAKINGNEWS100.jpg

Leave A Reply