Ommy Dimpoz afanikisha uzinduzi wa video yake

1Ommy Dimpoz akiongea jambo wakati wa sherehe za uzinduzi wa video ya wimbo huo.

2Mrembo aliyewahi kushiriki kwenye Big Brother Africa enzi hizo Abby akimpa kampani Ommy Dimpoz kwa kucheza kwenye uzinduzi huo.

3Vanessa Mdee akiwa kwenye pozi mara baada ya kuwasili ukumbini hapo.

4Wasanii wa Bongo Fleva Joh Makini na Ben Pol wakiwasili ukumbini hapo.

5Baadhi ya warembo waliojitokeza kushuhudia uzinduzi huo wakiwa katika pozi.

6Christian Bella akiimba kwenye uzinduzi huo

7Mtangazaji wa Clouds FM Millard Ayo akimhoji jambo mmoja wa wasanii wa Bongo Fleva, Madee.

8Ommy Dimpoz akimshukuru Bella wakati akiimba kama moja ya kumsapoti.

9Baadhi ya mashabiki waliohudhuria ukumbini hapo wakifuatilia kwa makini zoezi la uzinduzi huo.

STAA wa Bongo Fleva, Omari Nyembo ‘Ommy Dimpoz’, usiku wa kuamkia leo alifanikisha uzinduzi wa kichupa cha wimbo wake mpya unaokwenda kwa jina la Achia Body.

Uzinduzi huo ilifanyika kwenye Ukumbi wa Akemi uliopo ndani ya jengo la Golden Jubilee Tower, ambapo ulihudhuriwa na baadhi ya wasanii wenzake kibao.

Wasanii waliojitokeza kumpa nguvu Ommy Dimpoz ni pamoja na Joh Makini, Ben Pol, Chege, Madee, Vanessa Mdee, Navy Kenzo Christian Bella na Mwana FA.

Habari/Picha: Musa Mateja/GPL

Loading...

Toa comment