visa

Ommy Dimpoz Apata Shavu NBA Marekani

MSANII wa Bongo Fleva, Ommy Dimpoz amepata mwaliko rasmi wa kuhudhuria michezo ya NBA All-Star ambayo itafanyika Chicago Marekani kuanzia Februari 14 hadi 16 mwaka huu.

 

Mastaa wengine kutokea Afrika waliopewa shavu hilo ni Sho Madjozi wa Afrika Kusini na Jidenna mwenye asili ya Nigeria na Marekani.

 

Mwaliko huo umetolewa na Chama cha Mpira wa Kikapu Marekani (NBA), kupitia NBA Africa ambao wamemgharamia kila kitu ikiwemo usafiri wa ndege na gharama za kuishi akiwa Marekani.

 

Ommy Dimpoz ameshare picha Kwenye Instagram akiwa kwenye ndege na Seven Mosha wakiwa njiani kwenda Marekani.
Toa comment