The House of Favourite Newspapers

OMMY DIMPOZ AREJEA NCHINI, ASIMULIA ‘KIFO’ CHAKE

MSANII wa muziki wa Bongo Fleva, Ommy Dimpoz amerejea nchini akitokea kwenye matibabu yake baada ya kuugua kwa muda mrefu alipokuwa amelezwa nje ya nchi.

 

Akizungumza katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere, Jijini Dar es Salaam wakati akirejea nchini Ommy Dimpoz amesema haamini kama amerudi nyumbani licha ya watu mbalimbali kumzushia kuwa amekufa.

 

“Hali kama unavyoiona mimi mwenyewe siamini naona nimefika nyumbani, kiukweli kuhusu uzushi wa kifo nishazoea kwa sababu ya kazi niliyoichagua inatufanya tuzoee hali kama hii. Lakini wanachojisahau duniani wote tunapita kila mtu atakufa na mimi nitakufa, kuhusu kuanza kuimba kwa sasa siwezi kuzungumzia chochote,” alisema Dimpoz.

Comments are closed.