The House of Favourite Newspapers

Omog Aanza na Washambuliaji Mtibwa

0

KOCHA Mkuu wa Mtibwa Sugar, Joseph Omog, ameanza kuisuka safu yake ya ushambuliaji inayoongozwa na Jaffar Kibaya, Salum Kihimbwa na Kelvin Sabato.

 

Msimu uliopita Mtibwa ilikuwa na changamoto kubwa kwenye safu ya ushambuliaji jambo ambalo liliifanya timu hiyo kupitia wakati mgumu kwenye Ligi Kuu Bara na kujikuta ikipambana kucheza mechi za mtoano kuepuka kushuka daraja.

 

Akizungumza na Spoti Xtra, Kocha Msaidizi wa Mtibwa Sugar, Awadh Juma, alifunguka kwamba: “Kocha Omog tayari ameanza kutoa programu mbalimbali kikosini ambapo ameanza na safu ya ushambuliaji ambayo imekuwa changamoto kubwa kikosini kwetu, tumekuwa tunatengeneza nafasi nyingi lakini tumeshindwa kuzitumia, hivyo mwalimu ameona aanze na hilo kwanza.

 

“Kwenye mechi mbili tulizocheza hatujafanikiwa kufunga bao lolote licha ya nafasi nyingi ambazo tumezitengeneza, hivyo ni lazima tulifanyie kazi kama benchi la ufundi kwani msimu huu ligi imezidi kuwa ngumu kutokana na ushindani kuwa mkubwa.”

HUSSEIN MSOLEKA, DAR

Leave A Reply