The House of Favourite Newspapers

Breaking News: Omog Afungashiwa Virago Simba

KLABU ya Simba leo Desemba 32, 2017 imeamua kuvunja mkataba na kocha wake mkuu, Joseph Omog ikiwa ni takribani siku moja baada ya vinara hao wa Ligi Kuu Tanzania Bara kuchezea kichapo cha bao 4-3 (penati) kutoka kwa Green Warious na kuwavua ubingwa wa Kombe la Shirikisho (FA).

HII HAPA TAARIFA YA MSEMAJI WA KLABU YA SIMBA, HAJI MANARA

=====23/12/201=====

=====TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI=====

Klabu ya Simba na kocha wake mkuu Joseph Omog, wameamua kwa pamoja kuvunja mkataba baina yao kwa makubaliano maalum yanayozingatia maslahi ya pande zote mbili.
Klabu inamshukuru kocha Omog na inamtakia kila la kheri kwenye maisha yake nje ya Simba.

Kwa wakati huu Timu yetu itakuwa chini ya kocha msaidizi Masoud Djuma na itaendelea na mazoezi kesho,na kupumzika siku ya Jumatatu kwa mapumziko ya sikukuu ya Christmas na itaingia kambini Jumanne kabla ya safari ya Mtwara,ambapo tutacheza na Timu ya Ndanda kwenye mchezo wa Ligi kuu wiki ijayo.

Pia kwa niaba ya uongozi, benchi la ufundi na wachezaji.tutumie nafasi hii kuwaomba radhi sana Wanachama na washabiki wetu kwa matokeo ya jana, sote tumeumia ila ndio mchezo wa mpira ulivyo, na tuwaombe muwe watulivu katika kipindi hiki ili tufikie malengo yetu.
Mwisho

Klabu inawatakia nyote Sikukuu njema ya Noeli na mapumziko mema ya wikiendi.

IMETOLEWA NA….

Haji S MANARA
Mkuu wa Habari Simba Sc

SIMBA NGUVU MOJA.

Kipigo cha jana cha Simba kilikuwa ni baada ya matokeo ya sare ya bao 1-1 katika dakika 90 za kawaida, ndipo mwamuzi Israel Nkono akaamuru zipigwe penati ambapo Simba waliambulia penati 3 na Green Warriors kupachika 4.

Omog ambaye ni Raia wa Cameroon alituwa Msimbazi mwaka jana na kusaini mkataba wa miaka miwili kuinoa klabu hiyo.

Comments are closed.