Onyo Kali La Celine Dion Kwa Drake

KWA mujibu wa Billboard, Drake aliwahi kuweka wazi kuhusu mpango wake wa kujichora tatoo yenye sura ya muimbaji  CelineDion. Septemba 18 kwenye intavyuu  aliyofanya na iHeratRadio.   Staa huyo wa ‘My Heart Will Go On’,  alimtaka Drake kuachana na mpango huo kwani hauna manufaa yoyote.

 

 

”Usifanye hivyo” aliongea kwa msisitizo. “Unaweza kuandika barua za upendo, unaweza kunitumia autograph kwa ajili ya watoto wangu, unaweza kunitembelea. Naweza kukualika nyumbani kwa ajili ya chakula cha mchana au usiku. Tunaweza kuimba pamoja. Chochote unachotaka hata kama ni kuongea na mama yako ili nikufurahishe,” aliwahi kusema Celine.

 

Celine amesema sura yake inabadilika jinsi muda unavyokwenda wala si kitu kilichokuwa kikitengeneza hela kwenye fani yake, anaamini tattoo yake kwenye mwili wa Drake haitakuwa na mwisho mzuri na kumfanya rappa huyo awe na muonekano wa ajabu atakapozeeka.

 

Drake anasifika kwa mahaba yake ya ajabu kwani kila anapomtunuku mtu huamua kuichora sura ya mhusika kwa mfumo wa tattoo.

Rihanna, LilWayne, Aaliyah na Sade ni miongoni mwa wanamuziki ambao Drake amewachora sura zao mwilini mwake.


Loading...

Toa comment