Hii ni Orodha ya Majina ya wanafunzi waliofariki dunia baada ya ajali mbaya kutokea wilayani Karatu.
Wanafunzi zaidi ya 32, wa shule ya St. Lucky Vincent Nursery & Primary School English Medium, walimu 4 na dereva wao wamefariki dunia baada ya basi la wanafunzi aina ya Coaster waliokuwa wakisafiria kuacha njia na kutumbukia mtaroni katika eneo la Mlima Rhotia wilayani Karatu Arusha wakati wakielekea kwenye ziara ya kimasomo.

Wanafunzi hao walikuwa wakienda Karatu kufanya mtihani wa ujirani mwema na wanafunzi wenzao wa Tumaini English Medium School ya Karatu.


