The House of Favourite Newspapers

Otilia live na Ally Yanga

0

OTII
Bendi ya ToT, Otilia Boniface akidendeka ‘live’ na shabiki maarufu wa Yanga aitwaye Ally Said ‘Ally Yanga’.

Richard Bukos, aliyekuwa Geita

KATIKA hali iliyoashiria usaliti, Jumapili iliyopita msanii wa Bendi ya ToT, Otilia Boniface alinaswa ‘live’ na shabiki maarufu wa Yanga aitwaye Ally Said ‘Ally Yanga’ wakibusiana.

OTII-2

Katika tukio hilo wawili hao walinaswa kwenye Viwanja vya Chato, mkoani Geita wakifanya usaliti huo huku Otilia na njemba huyo wakidaiwa kuziacha familia zao jijini Dar.

Wakiwa kwenye starehe zao, paparazi wetu aliliona tukio hilo na kuanza kuwafotoa picha ambapo Ally Yanga aligeuka mbogo na kuanza kumchimbia mkwara paparazi wetu.

“Ebwana mambo gani sasa hayo hebu futa picha hizo haraka sana tusije kuharibiana, mimi nina mke wangu naye ana mumewe hivyo hizo picha zitatuharibia,” alisema Ally Yanga.

Akizungumza na paparazi wetu, Otilia alisema katika tukio hilo walikuwa wakisalimiana tu na hakukuwa na dhamira nyingine kwa kuwa kila mmoja ana  ndoa yake.

Mmoja wa mashuhuda wa tukio hilo alisikika akimtaja Ally Yanga kuwa ni mkali wa ‘totoz’ hivyo mume wa Otilia huko aliko alie tu.

“Yule jamaa ni fundi bwana usimuone vile, mkeo akinasa pale hatoki, halafu nasikia jamaa anahonga balaa, mume wa Otilia akae chonjo tu,” alisikika shuhuda huyo ambaye alikataa kutaja jina lake.

JIUNGE NA GLOBAL BREAKING NEWS!

Leave A Reply