Oya masela mchezo huu hauhitaji hasira!!
Mambo veepe masela wangu? Ebana ndo kama hivo mtu fedenge ndo hivo mitikasi inaendelea kama dawa kama kawiz ama nene majembe yangu ukwehe? Basi ni mpango mzima, kaa humu mwanakwetu upate vitu adimu vya tauni bana. Kwani kuna chama letu ambaye kimeo chake cha foni kimezimwa? Kachala wako mi nateleza tu arifu kumbe kilongalonga changu ni orijino.
Basi bana, huku na huku juzikati f’lani hivi mtu mzima nilikuwa natokea kitaa cha Roki Siti kutimba skani la kusaka ugali yaani Bongo tambarare! Hapo ndo stori moo ya tudei inapoibukia chalii angu!
Ebana ilikuwa alfajiri f’lani hivi ameizing kibaridi kwa sana tu. Kitu kikanyanyuka hichooo kinaliacha Jiji la Miamba kwa mwendokasi. Si ndo kaka mkubwa napokea kisa kimoko hatare kinoma aisee kutoka tauni la wagumu Moshi moja hiyo!
Imekaaje sasa? Eti mazee usipotimba kwenye maishu ya kijamii, adhabu yake unakula bakora za kutosha aisee na unatakiwa usimaindi eti wanangu wenyewe wanasema mchezo huu hauhitaji hasira!!!
Sasa bana si ndo ukatokea msiba wa mwana kitaa cha hapo Moshi? Chama langu Mangi mwenyewe akaendelea na bata zake za kufa mtu na totozi wakare hadi aibu! Kumbe bana masela walikuwa wakimlia taiming na kummaindi ileile.
Mazee unaambiwa baada ya mitikasi yote ya prosesi za mazishi ndo ikatimba mida mibovu ya naiti. Machalii wakaona isiwe kitu, wakamuibukia kachala kwa fasi ya geto dheni wakampa bakora za kutosha ili iwe fundisho kwa wana wengine ambapo huwa wanabonyea inapokuja ishu ya kushiriki kwenye mbishe za kijamii kwa fasi ya kitaani.
Ebana hii ni sistimu ambayo imezoeleka huko kwenye mji wa wagumu kozi naminywa na wana hapa kuwa kuna mwana alikwapua kitu cha kuku dheni maraia wenye mahasira wakampa mbata hadi akavuta aisee. Dah! Kiukweli kama stori hiyo ni ya ukweli siyo mpango kabisa maana huko ni kuchukua sheria mkononi wanakwetu.
Masela mimi nasapoti pipo kula kitu cha adhabu kwa kukacha mbishe za kijamii za pamoko ili kuleta piisi kwa skani bati mambo ya kumpa mtu mbata hadi anafutika kwenye sura ya dunia ni ishu fekelo kinoma wanangu.
Ebana washkaji zangu mmenisoma? Kama veepe tuendelee kukaza wanangu.