The House of Favourite Newspapers

Oya mwana Dom tunakuja, umeshindwa penalti, kona utaweza?

0

Oya masela inakuwaje hapo kitaa cha Dom? Ndo kama hivo tunahamia suuni so kaeni mkao wa kumpokea Mpeke! Pande hizi ni mpango mzima arifu. Sema tu kama ulivyosikia, kitaani ni mwendo wa kula wepesi tu kozi laifu linazidi kutaiti deili.

Kuna ishu moko mameni na maduu niliwahi kuwasanua hapahapa kwa fasi ya jamvini kuwa hivi wanangu inakuwaje shori yupo kwenye mambo yake ya gizani dheni anakubali mapichapicha ya maselfie na kachala akiwa na suti ya kuzaliwa? Unaona sasa kinachohapeni ni kwamba wash’kaji fyatu wanaamua kutupia tu kwenye mainsta na wasapu ili kukomoana dheni inakuwa imekula kwa shori. Huo si ndo umbulula wanakwetu? Kama veepe tupa kule ishu za kiloko.

Enewei, stori letu la tudei siyo hilo bati nimeona niwakumbushe tu maana si ndo sehemu ya laifu letu kusanuana wanangu? Dom mpo? Basi bana, jamaa yangu Debe Gwara kwa fasi ya kati ya Dom ananiteli kuwa ana mai waifu wake ambaye hapa tunapochitichati wana mkidi mwenye eji ya miezi bee na siku f’lani hivi. Basi bana unaambiwa wakati shori anajifungua, chalii aliona bora akashushie injini kileji kwa maza wa selaa. Sasa hapo ndo kuna bonge moko la kisa na mkasa.

Unaambiwa shori hakuweka mgomo wala nini badala yake akatimba kwa wakwe. Mzee mzima si ndo ikawa kama vile fungulia mbwa? Inaitwa weka mbali na makidi!

Kweli manzi akamaliza miezi bee kileji dheni akarejea tauni kulisongesha laifu na mjanja wake. Unajua mama alipotimba kwa mahomu kwa faza mtoto wake alichokutana nacho? Ebana ni fulu kwere.

Mastori aliyokutana nayo kwa majirani ni kwamba mwanangu mwenyewe alikuwa ni bandika bandua ya totozi hata tatu kwa naiti moko na ukizingatia yupo njema kimkwanja.

Sasa bana, kuna dei mmoko wa vichenchede wa selaa aliibuka maskani na kukutana feisi kwa feisi na mai waifu wa jamaa. Mazee unaambiwa palichimbika kinoma kozi yule mpango wa kando alimteli mai waifu wa jamaa kuwa kama penalti ilimshinda angeweza kona? Zile mboyoyo mingi ndo zilimpandisha mizuka yule waifu wa jamaa na kujikuta akitaka kumdedisha mchepuko laivu.

Bigi apu ziende kwa majirani waliookoa jahazi kozi tudei tungekuwa tunazungumza kitu ingine.

Mmenisoma wana? Kama vepe sii yuu neksti wiki. Dom tunaibuka eni taimu! Kwa komenti au kuchati na Mpeke, tupia kitu cha SMS kwa foni hapo juu.

Leave A Reply