The House of Favourite Newspapers

Oya mwana… kaza buti safari ni ndefu!

0

mmpeke-copyInakuwaje masela wangu wa kitaa hicho? Kipande hii ni gudi au guda kabisa wanakwetu. Ebana tangu nimebonyea lasti wiki naona kama nimewamisi kinomanoma watu wa Saa Godi. Au ninyi hamjanimisi nini na nini, mbona naona dizaini kama mnanifungia tu vioo makachala wangu wa ukwehe?

Pamoko na laifu kuwa tafu kitaani bati sisi hakuna kusanda wanangu. Kinachomata ni kukaza kitu cha buti dheni tusonge fowadi kozi bado safari ni ndefu ileile mazee.

Basi bana mwanangu Tii mwenyewe yupo kwenye taimu ngumu kimtindo kozi amefanya mautafiti na kunyaka kuwa kifaa chake cha maana yaani sumu kabisa anazingua aisee arifu.

Hebu imajini mtu anampiga usopusopu wa hatare dheni anagundua kuna wana f’lani hivi wa kitaa wanamlia vyake! Mbaya zaidi akimtaiti shori anachomoa wakati msela ana maushahidi yote. Huko si ni kutafutana ubaya machalii wangu?

Chama langu anakuteli kuwa anamzimika manzi wake kiasi kwamba hazipiti dakika bee bila kumuwaza na kurimemba mavituzi yake kozi shori naye kwenye yale mambo ya gizani ni faya. Kachaa anakuambia kuwa mbebiz wake mkare huwa hana longolongo anapokuwa kwa fasi ya graundi pale maeneo ya kumi na nane.

Baada ya kuhaso naye na kuona kifaa chake hakisomeki na ni sikio la kudedi dheni amefanya kila dizaini ili ammwage bati amefeli so yupo njia panda kozi hajui afanyeje?

Jamaa yangu kila akijaribu kujitoa kitu cha fahamu ili kujifogetisha, anasafa ile mbaya ndani kwa ndani. Mazee hapana chezea maumivu ya kitu cha moyo kozi wenyewe wanakwambia moyo mashine!

Kwa maushauri ya kitu cha Mpeke ni kwamba awe bize na jobu, chachi kwa sana na matizi dheni atafute masela wenye positivu maindi ajichanganye nao kitaa tofauti kabisa kuliko kuendelea kusebenza kitaa kilekile kitakachomfanya akumbuke machungu ya shori.

Mambo ya kujiulizauliza kwa nini mkaksi wake anamzingua atupe kule. Pia ni beta kucheki na kitu cha afya kama kipo poa dheni ajue dizaini ya kujitunza. Wanangu pigeni mbishe zote bati afya ikizingua ni mwisho wa mbwembwe zote.

Cha kufanya unapomingo na situwesheni kama hiyo ni kubonyea tu kisha kukaza buti kozi safari ni ndefu na watoto wapo kibwena wewe meki bingo tu uone, watakuja wenyewe wala hutatumia nguvu kubwa.

Mmenisoma? Kama vipi tunyakane hapa kwa fasi ya jamvini neksti wiki. Tchao!

Leave A Reply