The House of Favourite Newspapers

Oya mwana sasa hivi cha kumwamini mtu ni salamu tu!

0

mmpeke-copyMambo vepe masela wangu wenyewe? Ndo kama hivo mtu mzima nimeshajimuvuzisha kwa jamvini. Oya mazee unakaribishwa kuunga tela. Msanue mwana amsanue kachaa wake kuwa masela watake wasitake lazima waunge tela kwa mjanja wao.

Ebana taimu inakata fasta so ngoja tupige mastori ya kuwapa faida wana ili wanapomingo na situwesheni dizaini kama hii dheni wajue namna ya kuchomoka.

Washkaji siyo sekreti kwenye deizi kama hizi, pipo wamelosti uaminifu kinoma kiasi kwamba kilichobaki pekee cha kuwaamini baadhi ya washkaji ni salamu tu mengine yote ni fiksi.

Kwenye mishe za kuchati na wanangu wenyewe jamaa yangu wa hapo Moro tauni akaona isiwe kitu. Akaning’ata kitu cha sikio kuhusu mkasa f’lani hivi unaomzingua.
Miaka bee iliyokrosi mnyama wangu alijikuta anafolu vibaya kwenye mambo f’lani na mtoto mmoko mkare aliyejaliwa umbile la kibantu. Kitu nachuro kala, cheusi mangala, mkidi kaenda kwa mahewa.

Mwanangu akaanza kuhudumia mgodi akitegemea utatema taimu yoyote. Kweli bana Saa Godi siyo kama Mpeke. Shori akaingia laini, msela akaanza kuchimba madini.
Huku na huku si mkiksi akanasa kitu cha preginanti. Jamaa fulu hepi akijua taimu siyo ndefu atakuwa faza nani.

Si unajua zile za kuwa hepi hadi unapitiliza? Auti za kufa mtu kwenye viwanja klaski hapo Mji Kasoro Bahari.

Huku na huku miezi tisa hiyooo ikakata dheni shori akajifungua bonge moja la jentromani. Yaani mwanangu akaangusha pati ya kufa mtu, watu wakapiga mpunga na bata za maana.

Ebana eee…jamaa yangu haamini kozi shori amemchenjia ile mbaya eti mtoto siyo mali yake na badala yake kapewa maprosoo mwenye kisu kikali.

Watu wanakuambia jamaa yangu anapoulizia mkidi wake anaambiwa aache mboyoyo mingi na kama akiendelea kuleta za kuleta basi ajue kuwa atapotezwa kwenye feisi ya dunia. Ungekuwa wewe ndo msela ungefanyeje? Niamini mimi, nawu deizi kuna baadhi ya wana hawaaminiki hata aseme nini. Ni mwendo wa kuzinguana mwanzo mwisho.
Mmenisoma washkaji? Kama vepe sii yuu neksti wiki.

Leave A Reply