The House of Favourite Newspapers

ads

Ozil Amwagia Sifa Ronaldo, Atoa Neno kwa Wachezaji wa Kizazi cha Sasa

0
Nyota wa Timu ya Taifa ya Ureno Cristiano Ronaldo anapitia kipindi kigumu katika mashindano ya Kombe la Dunia nchini Qatar akiendelea kusota benchi

NYOTA wa zamani wa klabu ya Real Madrid, Arsenal pamoja na Timu ya Taifa ya Ujerumani Mesut Ozil ameibuka na kusemam kuwa Cristiano Ronaldo ndiye mchezaji mwenye mafanikio zaidi Duniani na kila shabiki wa soka duniani anapaswa kujisikia furaha kumuona akicheza soka kwa zaidi ya miaka 20.

 

Ozil ametamka maneno hayo wakati huu ambao nyota wa Timu ya Taifa ya Ureno Cristiano Ronaldo amekuwa katka wakati mgumu akiendelea kusota benchi katika kikosi cha Fernando Santos kinachoshiriki mashindano ya Fainali za Kombe la Dunia nchini Qatar.

Ozil amemkingia kifua Ronaldo

“Kila shabiki wa soka anapaswa kujisikia furaha kumuona Cristiano Ronaldo akicheza soka la kiwango cha juu kwa miaka zaidi ya 20. Sidhani kama kuna mtu kwa kizazi cha sasa anayeweza kufikia namba zake. Daina atakuwa kwenye kipengele chake pekeyake.” amesema Ozil.

 

Cristiano Ronaldo na timu yake ya taifa ya Ureno wanatarajia kushuka dimbani siku ya kesho kuvaana na Timu ya Taifa ya Morocco katika mchezo wa mtoano wa hatua ya robo fainali.

Leave A Reply