The House of Favourite Newspapers

Ozil Nina Furaha Arsenal

Na Mwandishi Wetu/ CHAMPIONI/GPL

KIUNGO wa Arsenal, Mesut Ozil, amesema kuwa ana furaha kwenye kikosi cha Arsenal kwa sasa.
Kumekuwa na kauli mbalimbali kuwa kiungo huyo anaweza kuondoka kwenye timu hiyo mwishoni mwa msimu huu pamoja na staa mwenzake, Alexis Sanchez, baada ya kugoma kuongeza mkataba.
Mkataba wa Ozil unatarajiwa kumalizika mwishoni mwa msimu ujao.
“Jambo la msingi ni kwamba bado nina mkataba kwenye timu hii ya London, kuzungumzia maisha yangu sasa halitakuwa jambo sahihi.
“Mwishoni mwa msimu huu mtaona nini kitatokea, tayari kutakuwa na mazungumzo mbalimbali, lakini kila mmoja anatakiwa kujua kuwa nina furaha Arsenal.
“Bado sijajua nini nitakachoamua lakini jambo la msingi ni kusubiri tuone,” alisema kiungo huyo wa zamani wa Real Madrid.

Comments are closed.