#GlobalCelebrities: P-Square Wanajua Kuishi Kistaa, Zicheki Picha Za Nyumba Yao Mpya

Wasanii wa Nigeria wanajua nini maana ya kuishi kistaa, na Peter na Paul Okoye maarufu kama P-Square ni miongoni mwa wasanii wanaojua kuitumia vizuri status yao.

Siku chache zilizopita nilikuambia ukitaka kujua msanii gani amefanya nini, wapi na lini isogelee Instagram au Twitter na huko utapata majibu ya maswali yako yote, sasa basi kwenye pitapita yangu Instagram asubuhi hii nimekutana na picha za mjengo mpya wa wakali kutoka Nigeria P-Sqaure.

Kwa mujibu wa baadhi ya mitandao ya Nigeria, P-Square waliamua kusherekea birthday yao ya kutimiza miaka 35 kwa kujizawadia jumba la kifahari na jana waliamua ku-share picha za nyumba yao na mashabiki. Ndani ya nyumba hiyo kuna sebule mbili kubwa, jiko kubwa la kisasa, chumba cha kuangalia sinema na sehemu ya kuogelea

Zicheki picha za nyumba mpya ya P-Square hapa chini.

IMEANDIKWA NA: Sandra Brown.

PICHA/ INSTAGRAM: Peter & Paul Okoye – P-Square.

Subscribe kwenye YouTube Chanel yetu ya Global TV Online ili zote kali zinazotufikia iwe ni siasa, michezo, comedy, burudani, stori za mastaamuziki na nyingine zikufikie kwa wakati.

 Tecno


Toa comment