The House of Favourite Newspapers

Pablo Ambadilishia Mbinu Nabi Yanga

0

 KOCHA Mkuu wa Simba, Pablo Franco, ameweka wazi kuwa atabadilisha mbinu zake kuelekea katika mchezo wa ligi kuu dhidi ya Yanga, unaotarajiwa kuchezwa Desemba 11 kwenye Uwanja wa Mkapa, Dar.


Licha ya Simba kuwa
na kibarua cha kumenyana na Yanga, lakini kwa sasa wanajiandaa na mchezo wa kimataifa dhidi ya Red Arrows ya Zambia, ukiwa mchezo wa marudiano wa Kombe la Shirikisho Afrika utakachezwa keshokutwa Jumapili nchini Zambia.


Kuelekea katika mchezo dhidi
ya Yanga, Simba wanakamata nafasi ya pili katika msimamo wa ligi kuu wakiwa na pointi 17 huku Yanga wakiwa vinara wa ligi hiyo wakiwa na pointi 19.

Akizungumza na Championi Ijumaa, Pablo alisema kuwa mbinu ambazo alizitumia katika mchezo uliopita wa ligi dhidi Geita Gold hatazitumia tena katika michezo miwili ijayo dhidi ya Red Arrows na Yanga kutokana na kushindwa kufanya vizuri.


“Tumefanikiwa kupata ushindi
dhidi ya Geita Gold, lakini hatukuwa na mchezo mzuri sana, tulicheza kwa kiwango
cha wastani, hatukuwa katika
muongozo mzuri wa muundo ambao nilikuwa nahitaji timu iweze kucheza.


“Bahati nzuri nimeligundua
hilo na nitakwenda kufanya mabadiliko ya mbinu kuelekea katika michezo yetu miwili ijayo dhidi ya Red Arrows na Yanga, mbinu ambazo nilizitumia hazitatumika tena katika michezo ijayo,” alisema kocha huyo.

STORI: MARCO MZUMBE NA HAWA ABOUBAKHARI, Dar es Salaam | CHAMPIONI IJUMAA

 


Leave A Reply