Pablo Amhofia Chama Shirikisho Afrika

KOCHA Mkuu wa Simba, Pablo Franco, ameichungulia droo ya hatua ya makundi ya Kombe la Shirikisho Afrika
na kufunguka kuwa,
wanatarajia kukutana na upinzani mkubwa katika hatua hiyo huku akimtaja Clatous Chama kama miongoni mwa mastaa hatari ambao inabidi wajipange kuwadhibiti.

 

Jumanne wiki hii droo ya hatua ya makundi ya Kombe la ShirikishoAfrika ilipangwa kwenye makao makuu
ya Shirikisho la Soka
Afrika (Caf), Cairo jijini Misri ambapo Simba wameangukia Kundi D pamoja na timu za RS Berkane ya Morocco, USGN ya Niger na ASEC Mimosas ya Ivory Coast.


Katika hatua hiyo, Simba
wanatarajia kuanza kibarua chao cha kwanza nyumbani kwenye Uwanja wa Mkapa, Dar es
Salaam ambapo
wataikaribisha ASEC Mimosas kutokea Ivory Coast Februari 13, mwaka 2022.

Akizungumza na Championi Ijumaa, kocha Pablo alisema: “Kwanza napenda kuweka wazi kuwa siwajui sana wapinzani tuliopangwa nao kwenye Kundi D la Kombe la Shirikisho Afrika, lakini najua kuwa tunakwenda kucheza dhidi ya timu ngumu kwani baadhi zimekuwa na rekodi nzuri kwenye soka laAfrika.


“Lakini pia
tutacheza dhidi ya timu kama RS Berkane ya Morocco ambayo ni miongoni mwa timu zenye wachezaji bora, najua hata Clatous Chama ni miongoni mwa wachezaji wanaocheza kwao na ni hatari, hivyo tunatarajia upinzani mkubwa lakini tunajiamini na tuna matumaini makubwa ya kufuzu.”

Stori: JOEL THOMAS, Dar es Salaam706
SWALI LA LEO

Kupanda Kwa Bei ya Mafuta Nchini, Nini Kifanyike Kupunguza Bei?
Toa comment