Na Issa Mnally, Risasi
DAR ES SALAAM. Mwanamuziki nyota wa FM Academia, Pablo Masai wakati wowote kuanzia sasa ataoa baada ya hivi karibuni kumvalisha pete ya uchumba, mpenzi wake wa muda mrefu, Shubi Peter.
Katika hafla iliyofanyika kwenye Ukumbi wa Hoteli ya Picolo, Kawe jijini Dar na kuongozwa na MC Charlz Baba, wanamuziki wa Kundi la Wazee wa Ngwasuma na wadau kadhaa wa muziki walimshuhudia mwimbaji huyo raia wa DRC, akiwathibitishia nia yake ya kuoa.
“Amekuwa mpenzi wangu kwa muda mrefu, kama ni kusomana tabia imetosha, leo ninamvalisha pete ikiwa ni ishara kuwa wakati wowote navuta kitu ndani,” alisema Pablo na kusababisha shangwe kubwa kutoka kwa waalikwa.