The House of Favourite Newspapers

Pacha wa Saido Kuanza Kazi Yanga

0

BAADA ya kuenea kwa tetesi nyingi juu ya usajili wa straika mpya wa Yanga, raia wa Congo, ambaye ni mchezaji wa zamani wa timu ya Angers ya Ufaransa, Ferebory Dore, anayetajwa kama pacha wa Said Ntibanzokiza ‘Saido’ anatarajia kutua nchini na kujumuika na kikosi hicho tayari kwa kuanza kazi.

 

Tayari Yanga wanadaiwa kumalizana na Dore kupitia kwa Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili ya Yanga, Injinia Hersi Said ambaye tayari ameshamaliza biashara na vibali vya mchezaji huyo, Dore mwenye umri wa miaka 31, akitokea Brazzaville, Congo.

 

Dore hadi anaingia rada za Yanga ni mchezaji huru pamoja na huko nyuma kuwahi kukipiga katika Klabu ya Angers ya Ufaransa.

 

Chanzo chetu makini kimeeleza kuwa, tayari Hersi amemaliza dili hilo na muda wowote kuanzia sasa ataanza kuchapa kazi hiyo baada ya taratibu za timu kuwasili jijini Dar es Salaam, ikitokea Sumbawanga walikokuwa na mchezo na Tanzania Prisons.“

 

Kwa sasa kila kitu kuhusiana na mchezaji huyo kimekamilika na kitu kikubwa ambacho kinasubiriwa ni timu kurejea Dar kisha yeye kuanza majukumu yake.“

 

Viongozi tayari wamemaliza kila kitu kuhusiana na vibali vyake na sasa ni yeye tu kujumuika na wenzake kwa ajili na kuanza kucheza,” kilisema chanzo hicho.

 

Hivi karibuni gazeti hili, lilimkariri Injinia Hersi akitamba kuwa wapo kwenye mazungumzo ya mwisho na mchezaji ambaye atakuja kuingia moja kwa moja kikosini jambo ambalo sasa limeanza kujidhihilisha kutokana na taarifa hizi.

 

Mbali na hapo Injinia pia inadaiwa kuwa anafi kiria suala la kumrejesha Heritier Makambo anayeitumikia Horoya AC ya Guinea kwa kuwa mashabiki wa Yanga wamekuwa wakionyesha kuwa na nia ya kutaka arejee klabuni hapo.Musa Mateja, Dar es Salaam

Leave A Reply