The House of Favourite Newspapers

Pacman, Nampepeche kupasuana kesho

MABONDIA wa ngumi za kulipwa nchini, Nasibu Ramadhani ‘Pacman’ na Issa Nampepeche kesho Jumamosi wanatarajia kupanda ulingoni  ugombania mkanda wa Ubingwa wa Afrika Mashariki na Kati katika pambano litakalopigwa kwenye Ukumbi wa Club 361, Mwenge Dar.

Mbali ya mabondia hao,wengine  watakaopanda ulingoni kesho ni bondia Tonny Rashid dhidi ya Haidari Mchanjo ambao watagombania ubingwa wa Afrika Mashariki na Kati wakati Seleman Kidunda atapanda ulingoni dhidi ya Nassor Hussein ikiwa ni maandalizi ya Michuano ya Majeshi ya Dunia itakayifanyika nchini China.

 

Mapambano hilo limeandaliwa na Club 361 kwa kushirikiana na PeakTime, Solid Rock huku likidhaminiwa na  Gazeti la  Michezo la Championi, Global Tv Online.

Mabondia hao leo wamepima uzito kwenye Ukumbi huo tayari kwa mapambano hayo ya kukata na shoka kutoka na  kila bondia kumtambia mwenzake kuibuka na ushindi kesho kesho kutokana na maandalizi waliokuwa wameyafanya.

Mapambano mengine ya utangulizi yatakuwa ni kati ya Lukmani Ramadhani dhidi ya Ismail Haridi, wakati Bakari Dunda atacheza na Kudura Tamimu.

Comments are closed.