The House of Favourite Newspapers

Pacome, Hafiz Konkoni Waanza Kazi Rasmi Yanga

0
Kikosi cha timu ya Yanga kilichoanza dhidi ya Simba.

WACHEZAJI wapya wa Yanga, Pacome Zouzoua raia wa Ivory Coast na Hafiz Konkoni kutoka Ghana, jana walianza kazi rasmi ndani ya kikosi hicho.

Pacome ambaye ni kiungo na Konkoni akicheza nafasi ya ushambuliaji, jana kwa mara ya kwanza waliitumikia Yanga katika mechi ya kimashindano, dhidi ya Simba ukiwa ni mchezo wa fainali ya Ngao ya Jamii uliochezwa Uwanja wa Mkwakwani, Tanga.

Hafiz Konkoni

Kuanza kazi kwa nyota hao, kunamaanisha kwamba wapo tayari kwa mikikimikiki ya msimu wa 2023/24 ambapo kesho Jumanne, Ligi Kuu Bara inatarajiwa kuanza, huku pia mastaa hao wakiwa na kazi ya kuhakikisha Yanga inatetea mataji iliyobeba msimu uliopita baada ya kuliachia Ngao ya Jamii lililobebwa na Simba.

Msimu uliopita, Yanga ilibeba Ngao ya Jamii, Ligi Kuu Bara na Kombe la Shirikisho la Azam Sports, huku ikicheza fainali ya Kombe la Shirikisho Afrika. Msimu huu watashiriki Ligi ya Mabingwa Afrika, wakiwa na malengo ya kucheza hatua ya makundi ya michuano hiyo.

Leave A Reply