Pacome Rasmi Abakia Yanga, Aongezewa Miaka Miwili

RASMI kiungo mshambuliaji wa Yanga raia wa Ivory Coast, Pacome Zouzoua ataendelea kubakia hapo katika misimu mingine miwili.
Kwa mujibu wa chanzo cha habari, juz kiungo huyo alisaini mkaraba huo wa miaka miwili baada ya kufikia makubaliano ya pande mbili Uongozi wa timu hiyo, na menejimenti ya mchezaji.
Chanzo hicho kilisema kiungo huyo amekubali kuongeza mkataba mpya baada ya kuboreshewa mahitaji yake muhimu ikiwemo bonasi na mshahara.