The House of Favourite Newspapers

Pah One washtukia wanapobugi

0

Pah One, Ola, Igwe na TabanakoWASANII wanaounda Kundi la Pah One, Ola, Igwe na Tobanako wameshtukia kitu wanachobugi na kushindwa kulikamata soko la Muziki wa Kizazi Kipya Bongo, wakisema sasa wameanza kujirekebisha kwa kukifanyia kazi ipasavyo.

Akipiga stori na Risasi Vibes kwa niaba ya wenzake, mmoja wa wanakundi hao, Ola alisema tatizo lao ni lugha ya Kiingereza wanayotumia katika nyimbo zao, kitu wanachoamini kinawakwamisha kwa vile mashabiki wao hawawaelewi hivyo wameanza marekebisho kwenye kibao chao kipya cha Zela, kwa kufanya kwa lugha ya Kiswahili.

“Tumeona hatueleweki sana Bongo kutokana na lugha ya Kiingereza tunayotumia ndiyo maana tumeamua kubadilika ili kuendana na soko la hapa,” alisema Ola.

Leave A Reply