PAKA WAAJABU AMTIKISA MCHUNGAJI

MOROGORO: Ukistaajabu ya Musa utayaona ya Firauni! Tukio la kushangaza lililotikisa mkoani Morogoro mwishoni mwa wiki iliyopita ni la paka wa ajabu kutinga katika eneo la kazi la mchungaji aliyefahamika kwa jina la Keneth Haule kisha kujificha kwenye droo iliyokuwa imefungwa na funguo. 

 

Paka huyo ambaye baadhi ya wananchi walimhusisha na imani za kishirikina alikutwa amejikunyata kwenye droo ya meza ambayo mtumishi huyo wa Mungu amekuwa akiitumia kutengenezea saa.

 

Siku ya tukio mwandishi wetu akiwa katika kutimiza majukumu yake maeneo ya Lunna, katikati ya Jiji la Morogoro, alishtushwa na umati wa watu uliokuwa umezingira eneo ambalo mchungaji huyo anafanya shughuli zake ambapo aliposogelea alipewa taarifa kuwa, ishu ni paka kukutwa kwenye droo katika mazingira ya kutatanisha.

 

“Bora umekuja ndugu mwandishi, ni hivi… huyu fundi hapa ni mchungaji pia, ana kanisa lake maeneo ya Tukuyu ingawa bado changa, mara nyingi huwa anatuhubiria hapahapa kijiweni.

 

“Sasa jana jioni alipofunga ofisi hilo droo lenye saa za wateja kalifunga na funguo vizuri kabisa, cha ajabu leo asubuhi alipofungua droo aanze kazi akakutana na paka ambaye kakodoa macho huku akiwa amejibanza pembeni kabisa.

“Kwa hali ya kibinadamu alishituka na kukurupuka, ndipo na sisi tukafika. Sisi wenyewe hatukuamini lakini tuliposogea ndiyo kweli tukamuona paka huyo, tulistaajabu sana.

 

“Unavyotuona hapa tunajiuliza huyu paka kaingiaingiaje humu kama hakuna mkono wa mtu? Tunahisi kuna watu wenye nia mbaya naye na hakika wamemtikisa,” alisema Rajabu Juma, mmoja wa madereva teksi waliokuwa wakimsaidia mchungaji huyo kumtoa paka huyo. Wakati mwandishi wetu akiendelea kutafuta undani wa tukio hilo, ghafla yule paka alikurupuka na kukimbia huku akiacha gumzo kubwa katika eneo hilo.

 

“Mhh! Makubwa… sasa huyu paka kaingiaingiaje humu jamani? Lazima kuna kitu… siyo bure,” alisikika mmoja washuhuda akistaajabu.

 

Akizungumza na Risasi Mchanganyiko, Mchungaji Haule alisema kuwa, alichokutana nacho kimemshitua sana kwani alishindwa kuelewa paka huyo aliingiaje kwenye droo hiyo.

 

“Mimi ni mchungaji, imani yangu sio haba na nimeshakemea tukio hili kwa jina la Yesu na kuvunja hila zote za shetani, hapa naendelea na kazi yangu kama kawaida ila kusema ukweli ni tukio ambalo limenitikisa, kama una imani ndogo unaweza kufunga ofisi.

 

JAMAA Aliyemkuna MAGUFULI Leo Ikulu “MUNGU Akufunike na MBAWA Zake”

Loading...

Toa comment