The House of Favourite Newspapers

Pam-D Alia Kutengwa na Wasanii Wenzake

Stori: Mayasa Mariwata | RISASI MCHANGANYIKO |Risasi Vibes

SEXY lady anayetamba na Ngoma ya Daffa, Pamela Daffah ‘Pam D’ Amelia kutengwa na wasanii wenzake kutokana na kuwa mpweke akidai wamemsusia shughuli ya arobaini ya baba yake aliyefariki dunia hivi karibuni.

Shughuli hiyo ilifanyika mwishoni mwa wiki iliyopita nyumbani kwao, Mbagala jijini Dar ambapo zaidi ya kaka yake Messen Selekta hakuhudhuria msanii mwingine yeyote.

Baada ya kuona hali hiyo, Risasi Vibes ilizungumza na Pam na kumuuliza kulikoni wasanii kutoonekana zaidi ya ndugu yake, ambapo alifunguka: “Kiukweli nimejisikia vibaya maana sikutarajia na ukizingatia wasanii wengi niliwataarifu, hapa ndiyo nimejua kwamba wasanii tuna urafiki wa kinafiki.

Comments are closed.