The House of Favourite Newspapers

Pam D: Kifo cha baba kimeniyumbisha kimuziki

Stori: MAYASA MARIWATA

MKALI wa Ngoma ya Nimempata, Pamela Daffa ‘Pam D’ ambaye hivi karibuni alipata pigo la kuondokewa na baba yake, Shedrack Nyato amesema kifo hicho kimemyumbisha kimuziki kwani alipanga kuachia ngoma mpya siku baba yake alipofariki.

Akipiga stori na Global Publishers, Pam D alisema, kwa kuwa siku aliyopanga kuachia wimbo ndiyo ambayo baba yake alifariki, huku yeye akiwa mtoto wa pekee  amejikuta kwenye wakati mgumu na kushindwa kupata maamuzi sahihi katika kazi zake za muziki.

“Sielewi nifanyeje kama niachie au la maana bado siko sawa na muziki unatakiwa uwe sawa kifikra, maana naweza kutoa ngoma nikapata shoo nikashindwa kufanya vizuri, naomba mashabiki wangu wanisamehe kwa hilo naamini ‘soon’ nitakuwa sawa na kuachia huo wimbo huo,”alisema.

Comments are closed.