PAM D KUTIMKIA SAUZ

SIKU chache mara baada ya kuachia Ngoma ya Umepenya akiwa amemshirikisha Mfalme wa Singeli, Selemani Jabir ‘Msaga Sumu’ staa wa Bongo Fleva, Pamela Daffa yupo mbioni kutimia nchini Afrika Kusini ‘Sauz’ na kujikita huko kimuziki.

 

Akichonga na Full Shangwe, Pam D aliyewahi pia kubamba na Ngoma ya Nimempata na Popolipopo alisema, tangu aanze muziki hii ni safari yake ya kwanza na yote hiyo imetokana na kuonekana na kusikika kimataifa.

 

“Kama nilivyoimba kwenye Umepenya, nimesikika na kupewa shavu na Wasauz kwa hiyo keshokutwa (Jumatano) naelekea Sauz kufanya nao ngoma na pia kufanya ishu zangu za kimuziki ambazo zitakuchukua muda mrefu kidogo,” alisema Pam D.

Mambosasa: Abdul Nondo Alikwenda Iringa kwa Mpenzi Wake