The House of Favourite Newspapers

Mama Salma Kikwete Apata Pigo – Video

MKE wa Rais Mstaafu, Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete, Mama Salma Kikwete ambaye pia ni mbunge wa kuteuliwa (CCM) amepata pigo kwa kuondokewa na baba yake mzazi, Mzee Rashid Mkwachu leo Alhamisi, Julai 19, 2018.

 

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na mjukuu wa marehemu ambaye pia ni Mbunge wa Chalinze, Ridhiwani Kikwete, msiba huo upo nyumbani kwa Dkt. Jakaya Kikwete maeneo ya Msasani jijini Dar es Salaam na mazishi yatafanyika kesho Ijumaa, Julai 20, 2018 katika Makaburi ya Kisutu majira ya saa 10:00 jioni.

 

Global Publishers inatoa pole kwa familia ya Jakaya Kikwete kwa kuondokewa na mpendwa wao.  Inna Lillahi wa inna ilayhi raji’un.

RIDHIWANI aelezea kifo cha Babu yake/Ratiba ya Mazishi

Comments are closed.