Pamba jiji fc yapata udhamini wa jezi
Kaimu Mkurugenzi wa jiji la Mwanza Frank Mvati (Katikati) akiwa na wakurugenzi wa Netsports baada ya kusaini mkataba huo.
KAMPUNI ya uuzaji na usambaji wa vifaa vya michezo Netsports ya Dar es salaam imeingia makubaliano ya utengenezaji na uuzaji wa jenzi ya Pamba Jiji Fc kwa mkataba wa miaka miwili.
Akizungumza mara baada ya kusaini mkataba huo Darisi Bujaga Mkurugenzi wa Kampuni ya Netsports amesema wameamua kuwekeza kwenye timu ya Pamba Jiji Fc kutokana historia ya klabu hiyo sambamba na ukubwa wake ambao umesababisha kuwa na mashabiki wa Asili.
Bujaga amesema hawakujiuliza mara mbili mara baada ya kuona Pamba jiji fc kwa siku za hivi karibuni ikipambana kurejesha makali yake na ujio wa uwekezaji katika klabu hii anaamini utaisaidia timu hiyo kufikia malengo na hatimaye kurejea ligi kuu msimu ujao.
Kwa upande wake Frank Mvati Kaimu Mkurugenzi wa Jiji la Mwanza ameipongeza Netsports kwa udhamini wa jezi za wachezaji na mashabiki ikiwa ni moja ya nguzo mkubwa katika kusaidia timu kufikia malengo yake.
Aidha Mvati pia ametumia mwanya huo kuwaalika wadau na wapenzi wengine kuona fursa hii na kuja kuwekeza Pamba Jiji maana maeneo ya kuwekeza bado yapo kama usafiri na mambo mengine.