The House of Favourite Newspapers

Pamba Wanaitaka Ligi kuu, waichapa Mashujaa, Matubaini kibao ligi Kuu.

0


Baada ya ushindi wa 2-0 walioupata Pamba  dhidi ya Mashujaa FC kwenye dimba la Nyamagana, Kocha wa Pamba FC Yusuph Chippo amesema katika michezo minne iliyosalia kabla ya ligi hiyo kumalizika wataicheza kama fainali ili waweze kupanda daraja kucheza ligi kuu Tanzania bara kwa msimu ujao Pamba baada ya ushindi wa Leo wamefikisha alama 51 kwenye nafasi ya Pili kwenye msimamo wa Ligi Daraja la Kwanza ( Championship) nyuma ya JKT Tanzania wenye jumla ya pointi 61.


.
Akizungumza na Global Publishers Kocha Yusuph  Chipo amesema wameweka malengo ya kushinda kila mchezo, na huu dhidi ya Mashujaa ulikuwa kwenye mpango wao licha ya kupata ugumu kidogo kupata ushindi “Namshukuru Mungu tumepata ushindi , mechi ilikuwa ngumu, Mashujaa walikuwa bora katikati, tulipoteza utulivu kipindi Cha kwanza, kipindi cha pili tulibadili mbinu na zilitusaidia kupata ushindi kwakua mchezo huu ulikua ndio wa maamuzi kwamba tunaweza kupanda daraja au la”

“Tuna vita kubwa na Kitayosce, tumepanda nafasi ya pili, tutapambana tumalize Salama mechi za mwisho, tukishinda zote hakika tutapanda Daraja” amesema Kocha huyo, Baada ya mchezo huu, Pamba imebakiza michezo miwili ya ugenini dhidi ya Mbuni FC na African Sports ya Tanga pia kwenye dimba lake la nyumbani imesalia mitanange miwili tu msimu huu ambapo watacheza na JKT Tanzania pamoja na Fountaini Gate na kwakua msimu huu Timu mbili za juu kwenye msimamo wa Championship zitapanda daraja Pamba italazimika kushinda michezo yote iliyobaki ili wapande daraja.

Leave A Reply