The House of Favourite Newspapers

Pambano La Antony Joshua ‘Live’ Kwese Iflix

KESHO ni kesho ambapo pambano la Mwingereza Anthony Joshua na Alexander Povetkin linatarajiwa kupigwa kwenye Uwanja wa Wembley huku likishuhudiwa moja kwa moja kwenye App ya Kwese Iflix pekee kwa kununua VIP pass itakayogharimu Sh 1,300.

 

Mashabiki wengi barani Afrika watashuhudia kupitia App ya Kwese Iflix na hii ni baada ya Kwese kufanikiwa kuonyesha mechi zote za Kombe la Dunia ambazo zilifanyika mwaka huu na kufuatiliwa na mamilioni ya mashabiki.

Joshua anayeshikilia mataji matatu kati ya manne makuu ulimwenguni katika uzito wa juu (IBF, WBA na WBO), atakabiliana na bingwa mwenzake, Povetkin raia wa Urusi, kesho Jumamosi.

 

Mkurugenzi Mkuu wa Kwesé Iflix, Mayur Patel amesema: “Tangu kuzinduliwa kwa Kwesé Iflix miezi mitatu iliyopita, imekuwa nia yetu kuwaletea wateja wetu michuano inayotazamiwa zaidi na burudani ya aina yake kwenye simu zao.

 

“Katika Kwesé iflix, tumejitolea kuwaletea wateja wetu upeperushaji murua kabisa wa moja kwa moja wa spoti kupitia App yetu iliyoboreshwa. Ni azimio letu kuwaletea mashabiki barani Afrika matukio ya spoti wanayotamani zaidi kwa urahisi.”

Comments are closed.