The House of Favourite Newspapers

Panga Lapita na Sita Yanga leo Jumanne Kusaka Ushindi Dhidi ya Dodoma Jiji

0

KUELEKEA usajili wa dirisha dogo hapa nchini unaotarajiwa kufunguliwa Desemba 16, 2022 hadi Januari 15, 2023, mastaa 6 wa Yanga wamekalia kuti kavu kutokana na rekodi zao kuwa hafifu uwanjani.

Timu hiyo inayonolewa na Kocha Mkuu, Nasreddine Nabi, leo Jumanne ina kibarua cha kusaka ushindi kwenye mchezo wa Ligi Kuu Bara dhidi ya Dodoma Jiji, unaotarajiwa kuchezwa Uwanja wa Liti, Singida.

Ni Gael Bigirimana, nyota ambaye hajawa kwenye kiwango bora ndani ya Yanga, huku akiwa hana nafasi kikosi cha kwanza kwa kuwa amecheza mechi tano pekee na kuyeyusha dakika 242.

Dickson Ambundo, staa huyu msimu huu hajawa na mwendo mzuri, amecheza mechi nne za ligi na kusepa na dakika 187 akiwa ametoa pasi moja ya bao.

Joyce Lomalisa, licha ya kufanya vizuri kwenye mchezo dhidi ya Singida Big Stars, bado anatajwa kuwa kwenye uangalizi mkubwa wa benchi la ufundi la timu hiyo kuhusu kiwango chake akiwa ametumia dakika 420 na ametoa pasi mbili za mabao.

Heritier Makambo, mshambuliaji huyu akiwa amecheza mechi nne, kasepa na dakika 243, hajafunga bao wala kutoa pasi ya bao na nafasi yake inatajwa kuchukuliwa na mshambuliaji chipukizi Clement Mzize.

Yusuph Athuman na Crispin Ngushi, hawajaonekana kwenye kikosi cha kwanza kwa kile ambacho kilielezwa kuwa hawakuwa fiti.

Timu hiyo imetinga hatua ya makundi Kombe la Shirikisho Afrika msimu huu na imeweka wazi kuwa inahitaji kufika mbali na kuboresha kikosi hicho kwa mujibu wa ripoti ya kocha.

Injinia Hersi Said, Rais wa Yanga, alisema kuwa mpango mkubwa kwenye mechi za kimataifa na zile za ndani ni kufanya vizuri, huku masuala ya maboresho ya kikosi hayo yakisubiri ripoti ya Nabi.

“Tupo kwenye mashindano ya kimataifa ambayo yanahitaji umakini mkubwa, kikubwa kwenye suala la maboresho ya kikosi chetu ni kuwa na wachezaji wazuri ambao watatupatia matokeo chanya, kazi bado inaendelea,” alisema.

KOCHA MUIVORY COAST ATAJWA SIMBA, PANGA LAPITA na 6 YANGA, SENEGAL WAANZA VIBAYA QATAR..

Leave A Reply