Papa Francis Amteua Askofu Nkwande Kuwa Askofu Mkuu Mwanza

KIONGOZI Mkuu wa Kanisa Katoliki Duniani, Papa Francis amemteua Askofu Renatus Nkwande kuwa Askofu wa Jimbo Kuu Katoliki Mwanza. Askofu Mkuu Mteule Nkwande alikuwa Askofu wa Jimbo Katoliki la Bunda tangu Februari 20, 2011.

Habari kutoka Makao Makuu ya Kanisa Katoliki, Vatican zilizonukuliwa na Idhaa ya Kiswahili ya Redio Vatican, zimesema Askofu Nkwande anakwenda kuziba nafasi iliyoachwa wazi, baada Papa Francis kumteua Askofu Yuda Thadei Ruwa’ichi kuwa Askofu Mkuu mwandamizi katika Jimbo Kuu la Dar es Salaam, Juni 21, mwaka jana.

 

Askofu Nkwande alipata Daraja takatifu la upadri Julai 2, 1995 1995 na Novemba 27, 2010 aliteuliwa na Papa Benedict XVI kuwa Askofu wa kwanza wa Jimbo Katoliki la Bunda.

 

Aliwekwa wakfu na Kardinali Polycarp Pengo, Askofu Mkuu wa Jimbo kuu la Dar es Salaam, kuwa Askofu wa Bunda Februari 20, 2011. Amepata uaskofu akiwa na miaka mitano ya upadri na uaskofu mkuu akiwa na miaka saba ya uaskofu. Nkwande alizaliwa Novemba 12, 1965, katika Parokia ya Sumve, Mwanza.

Loading...

Toa comment