The House of Favourite Newspapers

Papa Francis Apimwa Corona

0

KIONGOZI wa KanIsa Katoliki Duniani, Papa Francis amepimwa virusi vya corona (covid-19) na kuthibitika kuwa hajaambukizwa.

 

Alipimwa virusi hivyo baada ya mmoja wa wachungaji anayeishi katika katika makazi yake kugundulika kuwa na virusi hivyo.

 

Vyombo vya habari nchini Italia viliripoti kuwa mchungaji huyo ambaye ni ofisa wa sekretarieti ya jimbo, aligundulika kuwa na virusi hivyo na kuzua hofu kuwa huenda Papa Francis naye ameambukizwa.

 

Kwa mujibu wa tovuti rasmi ya Vatican, mchungaji huyo alikuwa mmoja wa washiriki wa karibu wa papa na sasa amelazwa katika Hospitalini ya Roma wakati idadi ya walioambukizwa katika jimbo hilo ikifikia watano.

 

Leave A Reply