The House of Favourite Newspapers
gunners X

Papa Francis asisitiza serikali za Ulaya lazima zifanye zaidi kuwahudumia wahamiaji

0

Papa Francis ametoa wito kwa mataifa ya Ulaya kuonesha uvumilivu zaidi kwa wahamiaji wakati wa ziara yake katika mji wa kusini mwa Ufaransa wa Marseille.

Akizungumza katika mkutano wa maaskofu na vijana kutoka nchi za Mediterania, Papa huyo alisema “wale wanaohatarisha maisha yao baharini hawavamii”.

Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron alikuwa miongoni mwa waliohudhuria hotuba hiyo.

Inakuja wakati mjadala wa uhamiaji ukiwa umetawaliwa na watu wengi waliofika katika kisiwa cha Lampedusa nchini Italia wiki iliyopita.

Waziri wa Mambo ya Ndani wa Ufaransa Gerald Darmanin, ambaye alimsalimia Papa alipowasili Marseille siku ya Ijumaa, alisema nchi hiyo haitakaribisha wahamiaji wowote wanaokuja kutoka kisiwa hicho.

Takribani watu 8,500 waliwasili Lampedusa kwa boti 199 kati ya Jumatatu na Jumatano wiki iliyopita, kulingana na Shirika la Kimataifa la Uhamiaji la Umoja wa Mataifa.

Matamshi ya Papa yalirejelea ujumbe wake siku ya Ijumaa kwamba ni jukumu la binadamu kuwaokoa wahamiaji wanaojaribu kuvuka bahari ya Mediterania.

Alionya serikali dhidi ya “ushabiki wa kutojali” na “kupooza kwa hofu”, akisema kwamba “watu ambao wako katika hatari ya kuzama wakati wa kutelekezwa kwenye mawimbi lazima waokolewe”.

RAIS SAMIA AMUONDOA MSIGWA MAELEZO, CHANDE AMTOA TANESCO, AMTUMBUA MKUU wa WILAYA MTWARA

Leave A Reply