The House of Favourite Newspapers

Pape Osmane Sakho: Tutachukua Ligi na Ligi ya Mabingwa Afrika Msimu Huu

0
Kiungo wa Simba mwenye tuzo ya bao bora la CAF, Pape Osmane Sakho mwenye mpira akifanya yake.

PAPE Osmane Sakho, kiungo wa Simba mwenye tuzo ya bao bora la CAF alilowatungua ASEC Mimosas msimu uliopita, Uwanja wa Mkapa amebainisha kuwa wanaamini watachukua taji la ligi pamoja na Ligi ya Mabingwa Afrika.

 

Leo Simba inatarajiwa kuvaana na Big Bullets ya Malawi kwenye mchezo wa awali wa Ligi ya Mabingwa Afrika na ule wa marudiano unatarajiwa kuchezwa Uwanja wa Mkapa, Septemba 18.

Sakho amesema: “Nina amini kwamba tutashinda taji la ligi pamoja na Ligi ya Mabingwa msimu huu kutokana na maandalizi ambayo tumefanya kwani tutajitahidi kupata matokeo kwenye mechi zetu.

 

“Kila kitu tunafanya kwa ajili ya mashabiki tunaomba waendelee kutuombea, unajua sio kitu chepesi kupata matokeo kwenye kila mechi na wao wanajua kwamba haitakuwa rahisi.

 

“Msimu uliopita ulikuwa mbaya kwetu ila msimu huu ninajua kwamba kuna kitu kitatokea ni suala la muda tu. Sikutarajia kupata tuzo lakini ilitokea na nilipata nafasi ya kuongea na Sadio Mane.

 

“Mane yule ni rafiki yangu na kaka yangu ananishauri vingi na hivi karibuni aliniambia inabidi niongeze zaidi bidii kwa ajili ya kuipa matokeo timu na kutimiza majukumu yangu,” alisema Sakho.

KOCHA JUMA MGUNDA AJIBU KUHUSU VYETI VYAKE, TAARIFA YA COASTAL UNION, PRESHA YA SIMBA…

Leave A Reply