PAPII KOCHA KURUDI NGWASUMA

Johnson Nguza ‘Papii Kocha

MKONGWE wa Muziki wa Dansi, Johnson Nguza ‘Papii Kocha’ amesema kuwa anatarajia kujiunga na Bendi ya FM Academia ‘Wazee wa Ngwasuma’ aliyokuwa akiitumikia kabla ya kupatwa na majanga ya kifungo cha maisha na baadaye kupata msamaha wa Rais Dkt. John Pombe Magufuli.  

Akipiga stori na Mikito Nusunusu, Papii Kocha alisema hafikirii kujiunga na bendi nyingine yoyote zaidi ya kurudi kwenye bendi yake hiyo ya zamani kwani bado anaipenda.

“Kwa sasa nafanya kazi ya muziki kwenye maonesho mbalimbali nikiwa na baba (Babu Seya) kama wasanii binafsi lakini nikishatulia vizuri natarajia kurudi FM Academia na sifikirii kujiunga na bendi nyingine tofauti na hiyo,” alisema Papii Kocha

Stori: Richard Bukos

Toa comment