#Part2: Mkasa Wa Kweli Wa Mtumishi Mathayo Aliyegeuzwa Fisi Abebe Maiti, Aomba Msaada – Video
Katika kijiji cha Balangda, wilayani Hanang’, mkoani Manyara, anaishi Mathayo Darema, mtumishi wa Mungu mwenye ulemavu ambaye miaka mitatu iliyopita alifunga ndoa iliyoibua mijadala na maswali mengi katika jamii.
Licha ya mashaka hayo, leo ndoa yake inaendelea kuwa imara, na familia hiyo imebarikiwa kupata watoto watatu.
Safari ya maisha ya Mathayo si ya kawaida.
Kupitia mahojiano maalum aliyoyafanya na mwandishi wa Global TV, @hoseaelnino, Mathayo anaeleza kuwa awali jamii ilikuwa haiamini kama anaweza kuwa na familia kutokana na ulemavu wake.

