Pascal Wawa Akubali Yaishe Simba SC

KIMEELEKA! Ndiyo utakavyoweza kusema kwa beki wa kati wa Simba raia wa Ivory Coast, Pascal Wawa ambaye wiki iliyopita alisaini mkataba wa mwaka mmoja kuendelea kukipiga hapo.Muivory Coast huyo ni kati ya wachezaji wanaotajwa kumaliza mikataba yao mwishoni mwa msimu huu.

 

Kwa mujibu wa taarifa ambazo imezipata Spoti Xtra, Wawa alisaini mkataba huo kwa siri yeye pamoja na viungo Said Ndemla na Hassani Dilunga baada ya kufikia muafaka mzuri wa kuendelea kukipiga hapo.

 

Mtoa taarifa huyo alisema kuwa Simba hivi sasa bado wanaendelea na mazungumzo na baadhi ya wachezaji wengine wanaomaliza mikataba yao ya kuichezea timu hiyo inayonolewa na Mbelgiji, Sven Vandenbroeck.Aliongeza kuwa, Wawa usajili wake ulipitishwa na kocha Sven ambaye amependekeza abakishwe katika kuiboresha safu ya ulinzi ya timu hiyo inayoongozwa na mkongwe Nyoni.

 

“Wawa ameongeza mkataba wa mwaka mmoja wa kuichezea Simba, hivyo ataendelea kuwepo hapa.“Usajili wa Simba hivi sasa unafanywa kwa siri kubwa, alisaini siku moja pamoja na Ndemla na Dilunga,” alisema mtoa taarifa huyo.

Mtendaji Mkuu wa Simba, Senzo Mazingisa, hivi karibu alitamba kuwabakisha wachezaji wote aliowapendekeza kocha ambao mikataba yao inamalizika mwishoni mwa msimu huu.

 

“Hakuna mchezaji yeyote atakayeondoka Simba kwa wale wote ambao tunawahitaji labda wale ambao hatuwahitaji ndiyo watakaoondoka,” alisema Senzo

STORI: WILBERT MOLANDI, DAR


Loading...

Toa comment