The House of Favourite Newspapers

Patakuwa Hapatoshi! Huku Fahyma Kule Paula, Rayvanny Apagawa

0

Patakuwa hapatoshi! Hivyo ndivyo unavyoweza kusema ambapo kwa mara ya kwanza,Rayvanny atakutana uso kwa uso na baby mama wake, Fahyma  katika event ambayo Paula Kajala naye atakuwepo!

 

Inafahamika kwamba Paula ndiye aliyevunja penzi la wawili hao na kusababisha Rayvanny ahamishie majeshi kwake, lakini baadaye ikaelezwa kwamba Chui ameamua kurudi kwa mzazi mwenzake, Fahyma baada ya kuzinguana na paula.

 

Watatu hao watakutana ‘live’, Jumapili hii mkoani Kilimanjaro ambako itafanyika shoo kubwa ya mastaa wa Bongo Fleva na Bongo Movies katika Ukumbi wa Hugo Gardens.

 

Mitandaoni tayari kumechafuka, wadau wakihoji je, Rayvanny atachagua kuhang na nani kati ya wawili hao?

R KELLY AHUKUMIWA MIAKA 20 JELA, SASA KUTUMIKIA KIFUNGO cha MIAKA 30, ATATOKA AKIWA na MIAKA 86

Leave A Reply