The House of Favourite Newspapers

Pato la Taifa laongezeka asilimia 6.7

benno-001Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT), Profesa Beno Ndulu (kushoto) akizungumza na wanahabari. Pembeni yake ni viongozi wa Benki Kuu.

BENKI Kuu ya Tanzania (BoT) leo imesema kuwa ukuaji wa Pato la Taifa umeongezeka na kufikia asilimia 6.7 ikilinganishwa na ongezeko la asilimia 5.7 kwa nusu ya kwanza ya mwaka 2015 kipindi kama hiki.

Akizungumza na wanahabari leo jijini Dar es Salaam, Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT), Profesa Beno Ndulu leo alisema shughuli za kiuchumi zilizoonekana kukua zaidi katika kipindi hicho cha nusu ya kwanza ya mwaka 2016 ni uchukuzi na uhifadhi wa mizigo asilimia 17.4, uchimbaji wa madini na gesi asilimia 13.7,  mawasiliano asilimia 13.0 na sekta ya fedha na bima asilimia 13.0.

Alisema ukuaji wa sekta ya uchukuzi na uhifadhi wa mizigo umetokana na kuongezeka kwa usafirishaji wa abiria kwa njia ya barabara na gesi, asilia ambao umekua kwa zaidi ya nusu ukilinganisha na robo ya pili ya mwaka 2015.

Aidha, alijata sekta nyingine ambazo zimefanya vizuri ikilinganishwa na kipindi kama hicho kwa mwaka 2015 kuwa ni sekta ya kilimo ambayo imekua kwa asilimia 10.3 kwa robo ya pili ya mwaka 2016 wakati mwaka jana ilishuka kwa asilimia 8.4.

Na Denis Mtima/Gpl.

 

Comments are closed.