The House of Favourite Newspapers

Patrick Aussems: Simba Kuna Viongozi ‘Waongo’

0

Aliyekuwa kocha wa Simba SC, Patrick Aussems ‘Uchebe’ Novemba 3, 2019 kupitia  ukurasa wake wa mtandao wa kijamii wa Twitter na Instagram,  amesema ili klabu hiyo, iendelee inatakiwa kuachana na viongozi waongo na wasiokuwa na uelewa katika bodi yake ya wakurugenzi.

 

Aussems kupitia mitandao hiyo amewaaga mashabiki na wachezaji wa Simba kufuatia kuondoka kwake nchini baada ya kumalizana na klabu hiyo.

 

Kocha huyo, Mbelgiji aliposti ujumbe huo, uliokuwa ukisomeka, “Asanteni mashabiki wa Simba. Nawatakia kila la kheri. Ili Simba ikue, lazima watimue waongo na watu wasio na elimu kwenye bodi ya wakurugenzi.”

 

Ujumbe huo, uliendelea kwa kusomeka kuwa sasa ni muda wa kufurahia na familia yake huku akimalizia, “Kwaheri Tanzania.” Kocha ameondoka akiicha Simba ikiwa katika kilele cha msimamo wa Ligi Kuu Tanzania Bara.

Leave A Reply