The House of Favourite Newspapers

Patrick Kanumba Afungukia Penzi Lake na Jennifer Kanumba – Video

Patrick wa Kanumba.

STAA kijana aliyetambulishwa rasmi kwenye ulimwengu wa filamu za Kibongo na aliyekuwa nguli wa tasnia hiyo, marehemu Steven Kanumba, Othman Yusuf maarufu kama ‘Patrick wa Kanumba’ amefunguka juu ya uvumi unaoenea ukidai yuko kwenye penzi zito na muigizaji mwenzake, Hannifa Daud ‘Jennifer wa Kanumba’ ambapo amekanusha vikali madai hayo.

Jennifer

Katika mazungumzo maalum na kipindi kinachojipatia umaarufu na kuvuna mashabiki kila kukicha cha Mpaka Home baada ya kuibukiwa nyumbani kwao usiku mnene, Patrick alikiri kusikia uvumi huo kupitia watu mbalimbali ambapo alisema yeye na Jennifer ni kama ndugu kwani hata familia zao zina uhusiano mzuri hivyo hawezi kufanya kitu cha ‘kijinga’ namna hiyo.

Kanumba enzi za uhai wake akiwa na Patrick na Jenifer.

Aidha amefungukia maisha yake wakati akiwa na Kanumba kabla ya kifo chake na maisha yake ya sasa baada ya kuondoka kwa nguli huyo wa filamu aliyemtengeneza na kulikuza jina lake.

MPAKA HOME: Twende pamoja umsikie Patrick alivyofunguka.

HADITHI: SIKU ZA MWISHO ZA UHAI WANGU – SEHEMU YA 1 (Audio)

Nakuletea dakika 15 za kwanza za simulizi hii tamu ya SIKU ZA MWISHO ZA UHAI WANGU. Ukitaka kuisikiliza simulizi hii Install #GlobalPublishersApp sasa. Utasoma na kusikiliza kitabu chote kuanzia sehemu ya kwanza hadi ya mwisho bureeeee!

Android: Bofya ==>http://bit.ly/2AAQe1d
iOS: Bofya ==>http://apple.co/2Assf4M

Comments are closed.