The House of Favourite Newspapers

Paula Awapiga Na Kitu Kizito, Kajala na Harmonize Wamwaga Baraka

0
Harmonize, Kajala Masanja na Paula wakiwa katika mtoko wa pamoja

PAULA KAJALA; ni mrembo maarufu kwenye mitandao ya kijamii (sosholaiti) nchini Tanzania ambaye anadaiwa kuwapiga watu na kitu kizito baada ya kuzindua duka lake la nguo, lakini kiasi cha shilingi milioni 500 alichotaja kuwa ni mtaji hakikuonekana.

 

Duka hilo alilolipa jina la Paulah’s Closet lilizinduliwa Ijumaa ya Agosti 5, 2022 maeneo ya Mlimani City (siyo ndani) jijini Dar es Salaam na kupewa baraka zote na mama yake, Kajala Masanja na baba yake wa kambo, Harmonize ambao walihudhuria tukio hilo lililopewa jina na Pink Friday.

 

Wengi wa wahudhuriaji walisema hakukuwa na kitu cha gharama alizotaja huku wengine wakidai ni utopolo mtupu kuanzia nguo zilizooneshwa.

Duka la Paula

Kitendo hicho kimeibua mjadala mzito ambapo Paula ameibuka na kuwajia juu wanaomsema ni muongo akisema; “Acheni makasiriko (tusi), la kwenu hata la milioni moja liko wapi (tusi).”

 

Hata hivyo, kwa wanaoona mambo kwa mtazamo chanya wamempongeza Paula kwa kuweza kumiliki duka hilo akiwa na umri wa miaka 20 tu huku kukiwa na warembo kibao mjini ambao wameishia kwenye kudanga tu.

Cc; @sifaelpaul

Leave A Reply