The House of Favourite Newspapers

Paula: Nani Kawaambia Nimeachwa

0

PAULA Kajala; ni mrembo maarufu Bongo hasa kwenye mitandao ya kijamii ambaye hivi karibu amerejea nchini Tanzania kwa ajili ya likizo akitokea masomoni nchini Uturuki anakosomea uuguzi.

Paula ambaye ni binti wa staa wa Bongo Movies, Kajala Masanja na prodyuza wa muziki nchini Tanzania, P Funk Majani alipata umaarufu zaidi baada ya kuweka wazi uhusiano wake wa kimapenzi na msanii wa Bongo Fleva, Rayvanny baada ya kusambaa kwa ile video yao mbaya.

Sasa; kumekuwa na tetesi nyingi kuwa huwenda Paula ameachana na Rayvanny kwani kwa muda mrefu hawajaonekana pamoja.

Baada ya Paula kurejea Bongo, Rayvanny amekuwa bize na shoo za nje ya nchi akiambatana na msanii Maluma wa nchini Colombia. Katika moja ya posti zake, Paula ameshindwa kuvumilia na kuvunja ukimya;

“Kwa nini mnaniandana mara ooh nimeachwa, nani kawaambia nimeachwa au mnasikiliza mauongo ya bibi yenu, hivi mnavyoniona kuna mwanaume anaweza kuniacha mimi?”

Kwa kauli hiyo, Paula anamaanisha watu waache kueneza habari za yeye kuachana na Rayvanny ambaye anatamba kwamba kamwe hawezi au hana ubavu wa kumuacha.

Hata hivyo, baadhi ya wafuasi wake wamemkumbusha Paula kwamba hata Fahyma ambaye ni baby mama wa Rayvanny alitamba hivyohivyo, lakini mwishowe aliachwa mchana kweupe na kubaki kulialia

Leave A Reply