The House of Favourite Newspapers

Pawasa Ampongeza Cannavaro

KOCHA mkuu wa timu ya Taifa ya mchezo la Soka la Ufukweni ‘Beach Soccer’ Boniface Pawasa amefunguka kuwa kitendo cha uongozi wa Yanga kumpa jukumu la umeneja wa timu hiyo, beki wake Nadir Haroub Cannavaro ni cha kupongezwa.

 

Akizungumza na Championi Jumatatu, Pawasa amesema kuwa Cannavaro amestahili kupewa nafasi hiyo kutokana na nidhamu, uzalendo na kujituma kuitumikia timu hiyo kwa kipindi kirefu bila kuwa na migogoro kama baadhi ya wachezaji wengine.

“Amekuwa kiongozi bora ndani na nje ya uwanja huku akitoa mchango mkubwa kwenye timu ya taifa lakini pia amekuwa tofauti na wachezaji wengi wakongwe waliopita klabuni hapo kwa kuonyesha uzalendo na kusisitiza nidhamu na uvumilivu kwa wachezaji pindi inapotokea sitomfahamu.

 

“Kwanza nimpongeze mdogo wangu Cannavaro kwa hatua aliyofi kia kwani ni matunda aliyoyavuna kutokana na mbegu bora ya nidhamu aliyoipanda, Cannavaro ni mtu aliyezaliwa kuwa kiongozi kila mtu aliona jinsi alivyoitumikia Yanga kipindi anacheza hivyo naamini atafi ka mbali sana hususani kwenye tasnia hii ya soka,” alisema Pawasa.

Issa Liponda, Dar es Salaam

Comments are closed.