The House of Favourite Newspapers

Pedeshee katunzi ataka DNA ya Tiffah

0

toto d

 Issa Mnaly na Musa Mateja

MAKUBWA tena! Wakati Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’ akijinasibu kuwa mtoto Latiffa ‘Tiffah’ ni damu yake, pedeshee maarufu Bongo, Muzamil Katunzi ameibuka na kumtaka staa huyo wa Bongo Fleva kupima kipimo cha vinasaba (DNA) ili kujiridhisha kama kweli ni damu yake, Risasi Mchanganyiko lina mchapo kamili.

tiffahMtoto Latiffa ‘Tiffah’

TUJIUNGE NA CHANZO

Kwa mujibu wa chanzo, pedeshee Katunzi amekuwa akitajwatajwa kuwa huenda mtoto huyo ambaye Diamond anajinasibu kuzaa na mfanyabishara maarufu Zarinah Hassan ‘Zari The Boss Lady’  ni wake, kwani Katunzi aliwahi kuwa na ukaribu na mwanamke huyo.

“Watu wanamtajataja sana Katunzi katika hili suala, hivyo huenda kuna ukweli maana si mnakumbuka Zari na Katunzi waliwahi kuwa klozi?

TIFFAH DIAMOND (2)Diamond, Zari na mtoto Latiffa ‘Tiffah’

ETI SURA NI KATUNZI MTUPU

“Mtafuteni Katunzi mumbane vizuri maana watu kibao wanasema sura ya Tiffah ni yeye mtupu, sasa hapa na hata picha zinazotambaa kwenye mitandao, wameunganisha picha ya Katunzi na Tiffah yaani damdam,” kilimwaga ‘ubuyu’ chanzo hicho.

ZARIKatunzi na Zari

KATUNZI ANASEMAJE?

Waandishi wetu baada ya kupenyezewa ubuyu huo, walilazimika kufunga safari hadi Mikocheni jijini Dar kwenye ofisi za pedeshee Katunzi kutaka kujua kama madai hayo ni ya kweli au la!

HUYU HAPA KATUNZI

“Kusema kweli mimi nilifahamiana na Zari kabla ya Diamond, ila ukaribu wetu uliisha pale tu niliposikia Zari anatoka na mdogo wangu Diamond, sasa sijui watu wanasema ninafanana na Tiffah kwa kigezo kipi, ila nadhani watu wamekuwa na hisia mbaya tu maana sina uhakika kama Zari anaweza kuwa na mtoto wangu na asiniambie maana hatukuwahi kukosana hata siku moja.

AMTAKA DIAMOND APIME DNA

“Kutokana na hili, ningependa tu kumshauri Diamond kama hatajali sana aende kupima DNA ili awe na uhakika na haya yanayozungumzwa maana bila kufanya hivi sidhani kama atakuwa kweli na amani moyoni mwake, kwani maneno siku zote huumba jambo, yawezekana kabisa Tiffah hana uhusiano na mimi lakini akafananishwa tu kwa kuwa kuna watu walikuwa wanafahamu juu ya uhusiano wangu na Zari,” alisema Katunzi.

DIAMOND SASA

Mapaparazi wetu baada ya kusikia maneno ya Katunzi, walimtafuta Diamond ambaye alisema yeye ataendelea kusimamia msimamo wake kwamba Tiffah ni damu yake na anashangaa jinsi maneno yanavyoibuka kila siku kuhusu mtoto wake.

“Mimi sioni sababu ya kujibizana na mtu juu ya Tiffah kwani kila mtu anaongea anavyojisikia,  na wengi wao wanatafuta niwajibu ili waweze kufanikisha azma yao, wananishangaza sana watu wa aina hii kila siku kuibuka na jambo,” alisema Diamond.

Leave A Reply